Mwimbaji
Mahiri wa muziki wa nyimbo za Kiroho a.k.a Injili,Rose Muhando akiimba
wimbo wake mpya wa Facebook na Twitter mbele ya mashabiki wake,katika
uwanja wa Kambarage mapema jioni ya leo mkoani Shinyanga,ikiwa ni sehemu
ya muendelezo wa tamasha la Pasaka.Tamasha hilo linaloandaliwa na Msama
Promotions Ltd kesho jumapili linaendelea katika uwanja wa CCM Kirumba
jijiini Mwanza,ambapo Nyota wa Nyimbo za Injili kutoka nchini Afrika
Kusini,Rebecca Malope atawatumbuiza wakazi wa jiji hilo sambamba na
waimbaji wengine..
Mwimbaji
wa nyimbo za Injili,Upendo Kilahiro akiimba mbele ya wapenzi wa muziki
wa injili ndani ya uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Sehemu ya wapenzi wa muziki wa injili wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo.
Upendo
Nkone,ambaye amejizolea sifa kubwa kwa kuimba nyimbo za kusifu na
kuabudu,akiwaimbisha mashabiki ba wapenzi wa muziki wa injili ndani ya
uwanja wa kambarage jioni ya leo.
Pichani
kulia ni Mwimbaji wa nyimbo za Injili,Upendo Kilahiro akiimba jukwaani
huku akiungwa mkono na waimbaji wenzake wa muziki huo,anaefuta ni
Tumaini Njole,Faraja Ntaboba kutoka nchini Congo DRC na Mess Chengula.
Muziki wa Injili ulikuwa umekolea hapa.
Mwimbaji
wa nyimbo za injili, Faraja Ntaboba kutoka nchini Congo DRC akiimba kwa
hisia kubwa mbele wakazi wa mji wa shinyanga waliojitokeza kwa wingi
kwenye tamasha hilo la muendelezo wa pasaka,ambapo leo Jumapili
watatumbuiza kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Walioguswa na nyimbo za injili walinyoosha mikono hewani
Mdauu akifurahia jambo huku akiendelea kuunza dvd za wasanii wa nyimbo za injili
إرسال تعليق