BODI YA WAKURUGENZI MUWSA WATEMBELEA VYANZO VYA MAJI HIMO NA MOSHI

Wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,(MUWSA)wakiingia katika gari tayari kwa safari ya kutembelea vyanzo vya maji .
Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka wakielekea kwenye vyanzo vya maji vinavyosimamiwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi, MUWSA.
Wajumbe wa bodi wakiongozwa na mwenyekiti wao Shally Raymond (shoto)wakushuka vilima na kuluka vijito hatimaye wakafika mto Ghona katika mji mdogo wa Himo ambako kuna chemichemi ya maji inayotumika kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo la himo.
Wajumbe wa Bodi waiangalia Chemichemi hiyo huku wakipata maelezo toka kwa mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Makamu mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,Profesa Faustine Bee akiwa juu ya Bomba  kwa lengo la kutizama kwa ukaribu  Chemichemi hiyo .
Wajumbe wakitizama Chemichemi.
Meneja rasilimali watu wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,Michael Konyaki akitoa maelezo kwa mmoja wa wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa mamlaka hiyo Hajira Mmambe.Wengine ni Meneja ufundi,Kibasa(shati nyeupe)meneja biashara John Ndetiko(mwenye suti)na meneja Biashara kituo cha Himo ,Sanagawe(shati ya Bluu)
Wajumbe wakiendelea kupatiwa maelezo.
Baada ya kutizama Chemichemi hiyo safari ya kurudi ikaanza kama kawaida kiongozi ,Mama Shally Raymond akaongoza safari ya kupanda kilima.
Baadae wajumbe wa bodi wakatembelea matenki ya kuhifadhia maji baada ya kusukumwa kutoka katika Chemichemi iliyoko mto Ghona na kupatiwa maelezo toka kwa mkurugenzi mtendaji wa MUWSA,Mhandisi Cyprian Luhemeja..
Wajumbe wa bodi wakahitimisha ziara yao kwa eneo hilo la Himo kwa kutembelea ofisi mpya za mamlaka hiyo kituo cha Himo.
Wakiwa Moshi mjini wajumbe wa Bodi walitembelea Chanzo kipya cha maji kilichopo mto Karanga ambacho kwa sasa ujenzi wake unaendelea.
Ziara hiyo ikahitimishwa kwa majumuisho yaliyofanyika katika ofisi za mamlaka hiyo zilizopo katikati ya mji wa Moshi.
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa taarifa mbele ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka hiyo.
Baadaye mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingra mjini Moshi,Shally Raymond pamoja na wajumbe wengine wa bodi wakapata fursa ya kuzungumza juu ya yale waliyoona wakati wa ziara hiyo.
Baaadhi ya wajumbe wa bodi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini.

Post a Comment

أحدث أقدم