Watu wa karibu na familia ya aliyekuwa star wa Fast and
Furious, marehemu Paul Walker wameamua kuuza magari 30 yaliyokuwa
yanamilikiwa na star huyo.
Kwa mujibu wa TMZ, magari hayo ni pamoja na BMW, Audis, Musgangs na
Porsches yakiwemo magari yanayotumika kwenye mashindano ya mbio za
magari.
Hata hivyo, wameeleza kuwa hawatahusisha jina la Paul Walker na
bidhaa zinazouzwa kwa kuwa wanaamini yeye pia asingependa kuona jina
lake linatumika kufanya bei ya magari hayo iwe juu au kuvutia wateja
zaidi.
Magari hayo yatauzwa kupitia mawakala maarufu wa minada.
Mali za Paul Walker zinakadiriwa kuwa na thamani ya $25 million na
mtoto wake wa kike Meadow mwenye umri wa miaka 15 ndiye aliyetajwa na
marehemu kuwa mrithi wa vitu vyote hivyo.
Wakati wa uhai wake, Paul alimtaka baba yake mzazi kusaidia katika kuhakikisha mwanae anahamishiwa mali hiyo.
إرسال تعليق