Wasanii wa kizazi kipya kutoka “TMK” Temeke jijini Dar es Salaam,
jana siku ya Jumamosi walikinukisha ndani ya Samaki Samaki mji kasoro
bahari mitaa ya Kidonda mjini Morogoro. Wakati watanzania wameelekeza
Masikio na Macho kwenye KTMA2014, wasanii hawa chini ya MXCarter
Entertainment wakishirikiana na NYUMBaNI Park Walifanya show kali kwa
ajili ya wakazi wa mjini morogoro ambapo walisheheni eneo la tukio
kushuhudia majabali hayo mawili yakiungurumisha ngoma zao mpya na za
zamani.
PICHA.
إرسال تعليق