Dalali: Nitachukua fomu ya Urais Simba Jumatatu


Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali.
Na Khadija Mngwai
HATIMAYE mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali ametoa tamko rasmi juu ya kuwania nafasi ya juu klabuni hapo ambayo sasa hivi inafahamika kwa cheo cha rais wa klabu na siyo mwenyekiti, akisisitiza kuwa keshokutwa Jumatatu ndiyo itajulikana.
Akizungumza katika mahojiano malaamu na Championi Jumamosi, Dalali ambaye alikuwa ‘bize’ na shule kwa miaka kadhaa, amesisitiza kuwa atachukua fomu kuwania urais ikiwa ataona hakuna watu wenye vigezo waliojitokeza kufikia keshokutwa.
Mgombea pekee ambaye kufikia jana mchana alikuwa amejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi ya urais ni Dita Tupa ‘Tupac’.
Dalali amesisitiza kuwa ikitokea wagombea watajitokeza na kuwa na vigezo basi ataachana na mpango huo na kama hakuna ataingia kazini mwenyewe.
“Bado sijachukua fomu yoyote ya kuwania nafasi ya urais lakini naangalia wakina nani wanachukua fomu ili niweze kujua nini cha kufanya, kwani nimesikia wajumbe sita wanataka kujitokeza kuchukua fomu hizo.
“Hadi ikifika Jumatatu nikiona hakuna mwenye kigezo cha kuwa urais basi nitajitosa mwenyewe na kuchukua fomu ili niweze kugombea, kwani tunahitaji mtu atakayerudisha umoja Simba kwa kuwa sasa kuna makundi saba.
“Makundi hayo yanachangia kuifanya Simba kuyumba na kutoshiriki michuano ya kimataifa kwa misimu mitatu mfululizo.
“Rais wa klabu anayetakiwa ni yule mwenye hekima na busala,” alisema Dalali.

Post a Comment

أحدث أقدم