Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Kassim Dewji.
Na Khadija Mngwai
ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Kassim Dewji, amefunguka kwa kuwataka Wekundu hao wa Msimbazi kutosajili mchezaji yeyote nje ya nchi.

Simba imemaliza Ligi Kuu Bara ikiwa nafasi ya nne ikiwa na pointi 38
nyuma ya Mbeya City yenye pointi 46 na kuifanya ishindwe kushiriki
michuano ya kimataifa kwa mwaka wa pili mfululizo.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Dewji alifunguka
kuwa Simba haitashiriki michuano ya kimataifa mwakani hivyo ni vema
kutoingia hasara ya kusajili wachezaji kutoka nje ya nchi.
“Kwa jinsi hali ilivyo Simba hivi sasa, ni vema kamati husika ikaachana na mpango wa kusajili wachezaji nje ya nchi kwani hawatakuwa na maana yoyote kwa kuwa haishiriki michuano ya kimataifa.
“Kwa sasa nguvu yote ielekezwe kwa wachezaji vijana kutoka mikoani ili waweze kuisaidia Simba na ikifanikiwa kufanya vizuri ndipo baadaye wakasajiliwe wachezaji wa kimataifa ambao wataisaidia timu huko mbeleni.
“Lengo la sasa ni kuhakikisha ifanye vizuri na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa,” alisema Dewji.

إرسال تعليق