Demarco, asema East African DanceHall Artists hawajulikani Kabisa Jamaica.

Demarco_Blonde1
‘Demarco’ ni mmoja kati ya wasanii wa Dancehall wanaofanya vizuri sana kwa sasa nchini Jamaica. Moja kati ya nyimbo za msanii huyo zilizompa umaarufu ni “Never Gonna Let You Go”, “She Can’t Wait”, “True Friend” na “Our World” aliyomshirikisha Elephant Man mwaka 2008. Wiki iliyoisha Demarco alikuwa na tamasha nchini Uganda, ambapo wasanii wengi wa reggae na dancehall wamekuwa wakienda sana nchini Uganda kuliko nchi zingine zote za Afrika Mashariki na hii ni kutokana na mtindo wa muziki huo unakubalika sana nchini humo.
Kabla ya kufanya tamasha hilo Demarco alihojiwa na kituo kimoja cha redio na kusema “Nilipofika hapa kila nyimbo ninayoisikia ni ya ‘Chameleone’ peke yake na sio nyingine.Nyimbo zenu zote (Dancehall) mlizosema zinafanya vizuri huku hakuna hata moja inayofanya vizuri au kujulikana nchini Jamaica na hata wasanii wa nyimbo hizo. Wasanii wa Dancehall wa hapa (Uganda ) wanatakiwa waende Jamaica wajaribu kutangaza muziki wao kama wanapenda kujulikana.”
Hii inaonyesha kuwa wasanii wetu wanatakiwa kuongeza juhudi za kuutangaza muziki wao kimataifa zaidi kama kweli tunahitaji Dancehall na Reggae kutoka Afrika Mashariki ifanye poa.

Post a Comment

Previous Post Next Post