
Kabla ya kufanya tamasha hilo Demarco alihojiwa na kituo kimoja cha redio na kusema “Nilipofika hapa kila nyimbo ninayoisikia ni ya ‘Chameleone’ peke yake na sio nyingine.. Nyimbo zenu zote (Dancehall) mlizosema zinafanya vizuri huku hakuna hata moja inayofanya vizuri au kujulikana nchini Jamaica na hata wasanii wa nyimbo hizo. Wasanii wa Dancehall wa hapa (Uganda ) wanatakiwa waende Jamaica wajaribu kutangaza muziki wao kama wanapenda kujulikana.”
Hii inaonyesha kuwa wasanii wetu wanatakiwa kuongeza juhudi za kuutangaza muziki wao kimataifa zaidi kama kweli tunahitaji Dancehall na Reggae kutoka Afrika Mashariki ifanye poa.
إرسال تعليق