Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida SACP, Geofrey Kamwela.
Na Nathaniel Limu, Singida
DEREVA
wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida Juma Juma (52)
amefariki dunia wakati akifanya mapenzi na mwanamke mhudumu wa baa
kwenye nyumba ya kulala wageni.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema tukio
hilo limetokea mei tatu mwaka huu saa nane za usiku chumba no.S.2 nyumba
ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Top Life New Kiomboi mjini.
Amesema
siku ya tukio,dereva Juma saa sita za usiku alimwaga mpangaji wake kuwa
anatoka mara moja na hatachelewa kurudi nyumba kwa kwa hiyo alifunga
mlango wa mbele ya nyumba.
Amesema
kuwa saa mbili baadaye Juma alionekana akiwa baa iliyoko kwenye nyumba
hiyo la kulala wageni iliyoko umbali wa mita 50 kutoka nyumbani kwake.
“Muda
huo Juma alionekana akiwa na mmoja wa wahudumu wa baa hiyo alitwaye
Agness Mayo (32) anayesadikika kuwa na uhusinao wa kimapenzi na
Juma.”,amesema.
Kamwela
amesema mhudumu huyo wa baa mpenzi wa Juma,alitoweka mei nne mwaka huu
baada ya kuaga kwamba anakwenda kanisani na kutorokea kusikojulika.Hata
hivyo,ufunguo wa chumba alicholala Juma zilikutwa chumba cha kulala
wahudumu wa baa.
Kamanda
huyo amesema kuwa toka siku hiyo ya mei tatu chumba alicholala Juma
hakifunguliwa hadi mei tano mwaka huu na ndipo mwili wa dereva huyo
ulipokutwa ukiwa umeharibika vibaya.
“Uchunguzi
zaidi wa tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta mhudumu
aliyetoroka ili ahojiwe na kisha kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazomkabili endapo atabainika kuhusika na tukio hilo”,amesema Kamanda
Kamwela
Post a Comment