Diamond alishinda tuzo 7 lakini ushindi wa Fid Q ndio ulioshangiliwa/furahiwa zaidi - KTMA 2014

 Usiku wa Jumamosi, May 3, Diamond Platnumz alithibitisha kuwa ndiye msanii namba moja Tanzania. Japo hili linafahamika tangu siku nyingi kutokana na mafanikio aliyoyafikia ambayo hakuna msanii wa Tanzania aliyewahi kuyagusa. IMG_9419
“7 Nominations, 7 Awards…thanks alot my die hard fans, My family, Management and strongly supporting Media…jus so you know, all these belong to you, am jus holding them…Next stop @Mtvbaseafrica Mama Awards let’s keep voting and go get them,” aliandika staa huyo baada ya ushindi wake.
Ushindi wa tuzo saba uliovunja rekodi ya KTMA, haujawashangaza wengi kwakuwa ‘My Number One’ ni wimbo mkubwa mno na haikuwa rahisi kwa msanii yeyote aliyetajwa naye kutunisha misuli.
Pamoja na Diamond kushinda tuzo zote hizo, ni ushindi wa tuzo mbili wa Fid Q ndio uliogusa mioyo ya watu wengi.
IMG_0824
Kwa miaka mingi, rapper huyo kutoka Mwanza anayeaminika kuwa mwandishi bora zaidi wa hip hop kuwahi kutokea nchini, alikuwa akitajwa na kukosa tuzo. Hali hiyo ilipelekea mashabiki wake mwaka jana kumpa tuzo yao wenyewe baada ya kukosa tuzo za Kili. Hivyo kwa wengi, ushindi wa Fid Q uliwafanya walale usingizi mnono kwa kuamini kuwa hatimaye ametendewa haki.
“Namshukuru Mungu kwa ushindi wa @FidQ sasa mwaka mtakaompa Tuzo Belle 9 nitatoa sadaka kabsaaaaa,”
alitweet muigizaji Elizabeth Michael aka Lulu.

Kabla ya hapo aliandika: Yaani nakukubali we kaka…hivo yani…!mm sio mgumu ila kwa kazi zako najigumusha sometimes…!am so so happy 4 you yani hongera. Hehehehe Asante blaza,cjui ulisikia kelele Zangu ulivyotangazwa mshindi!?dah acha Leo nifunguke sio sababu ya Tuzo..yani ya moyoni tu
Ushindi wa Fid Q uliufanya ukumbi wa Mlimani City kulipuka kwa shangwe na vigelegele na huku wengine wakitamani kumbeba juujuu. Hata wasanii wenzake pia waliokuwepo ukumbini, walionekana kuwa na nyuso zenye furaha baada yam kali huyo kushinda tuzo hizo.
Yeye mwenyewe pia furaha ilikuwa kubwa kiasi cha kuishiwa hata maneno ya kuongea na kwa mara ya kwanza Ngosha alionekana kulengwa na machozi, machozi ya furaha. Twitter ililipuka kwa shangwe na ni ushindi wa Fid ndio ulioandikwa zaidi kwenye mtandao huo wa kijamii.
Hizi ni baadhi ya tweets:

BABA BOI ‏@Vickyulemmoja
If @FidQ would not have won that hiphop award,i would have been really disappointed.mad love bro kubanda

Rodgers Israel ‏@nelsonkivuyo
Kama kutenda haki basi mwaka huu #KTMA2014 wametenda haki sana kwani @FidQ ametendewa haki yake ya muda mrefu .. Big up bro keep it up

Khalef Rashid ‏@al_zaraay 19h
Feelin happy n excited as if I was the one who won the award..congrats bro @FidQ #mwanzamwanza #ngoshathedon #pamoja

ScoobyAskariWaMiguu® ‏@incredible_nory
Congrats Comrade @FidQ ..I knew u’d bring it home;jana mi nilikamatwa na homa moja matata just before seing you grab that award!! So Happy!

JOSEPH CHUWA ‏@joschuuurh
Conglats Ngosha The Don @FidQ on this one….finally you got what you deserved for a long time. pic.twitter.com/SVEVz62bdk

Z Tengimfene ‏@tangyjive
On other important news congratulations to @FidQ for the award, wish you could distribute your music in Mzansi as well.

Babu Sikare ‏@AlbinoFulani 23h
Nikuwa na furaha mpaka nikashindwa kupiga picha na wewe jana! Leo everything on me @FidQ ili tupige picha lol. #BestHipHopArtist

Maryam ‏@Toxeeqation May 4
I am happy you got the award.. @FidQ Congratulations.. ‘Been a long time coming…

grace kay ‏@AnotherKOT
Now I can sleep. Prayers didn’t go in vain. Congratulations once more @FidQ

Batuli_Actress ‏@Batuli223
@FidQ Congrarulations broda

Post a Comment

أحدث أقدم