Rappers Diddy, Rick Ross, Dr Dre, Nick Cannon, bondia Floyd
Mayweather na malkia wa talk show, Oprah Winfrey ni miongoni mwa mastaa
wa Marekani walioonesha nia ya kutaka kuinunua timu ya mpira wa kikapu
ya Los Angeles Clippers.
Hatua hiyo imekuja baada ya aliyekuwa mmiliki wa timu hiyo Donald
Sterling kupigwa marafuku katika maisha yake kujihusisha tena na
shughuli za NBA kwa kutoa kauli ya kibaguzi wa rangi. Ingawa bado
anaendelea kuwa mmiliki wa timu hiyo, kuna uwezekano mkubwa
akalazimishwa kuiuza kwa watu wengine.
Orodha ya watu wanaotaka kuinunua timu hiyo imeendelea kuongezeka
wakiwemo pia bondia Oscar De La Hoya, Magic Johnson na CEO wa zamani wa
Microsoft, Steve Ballmer. Oprah alitangaza jana kuwa yupo kwenye
mazungumzo na wafanyabiashara David Geffen na Larry Ellison kuweka dau
kuinunua timu hiyo.
Post a Comment