Exclusive:- At Na Hammer Q Wasema Kuna Siri Kubwa Katika Kundi La Offside Trick (audio)

Wasanii kutoka Zanzibar, AT na Hammer Q ni miongoni mwa wasanii ambao waliwahi kufanya kazi ya muziki wakiwa ndani ya kundi maarufu la muziki wa mduara la Offside Trick.

Wasanii hao ambao hivi sasa wanaendelea kufanya kazi kama Solo artists wameiambia tovuti ya Times Fm kuwa kuna siri kubwa katika kundi hilo na kwamba siri hiyo ndio chanzo cha kuvunjika.
Wakiongea kwa nyakati tofauti, wasanii hao wamesema kuwa picha inayowaonesha wakiwa wawili na ikiwa na neno ‘Siri.. loading’ sio wimbo wa pamoja bali ina maanisha kuna ‘siri’ na ipo siku wataiweka wazi.
“Hiyo kitu siri, ni kwamba kila mmoja ana siri yake ambayo kaikuta pale. Kila mmoja atapata muda wake siku muafaka kuweza kuelezea, kwa sababu vile langu limeshakuwa na la kwao limeshatokea kwa hiyo wao wenyewe watakuwa na vitu vingi vya kuelezea halafu baadae kila mmoja ataelezea kwa upande wake kwamba ni kitu gani kilichomfika...” AT ameiambia tovuti ya Times Fm.
“Mimi nakumbuka siku za nyuma nilisema, mimi siongei vitu vingi. Itafikia siku ntakuja kuongea vitu ambavyo vipo kabisa reality, hivyo nikivizungumza sitakuja kuonekana mimi nimemuonea Lil Ghetto lakini kwa sasa hivi bado mapema waache waende. Ndio maana akaenda Hammer Q kafeli na wengine wameshafeli.
“Sasa kinachofuata...siku nikija kuzungumza mambo yale ambayo yapo isije kuonekana kama yule bwana mdogo mimi namuonea, isipokuwa ni reality. Kwa sababu nyumba kwa nje ukiona imepakwa rangi unawezakusema nzuri lakini aliyekaa ndani ndiye anajua…mimi ipo siku ntakuja kuitoa hiyo siri, soon tu.” Ameesema AT.
Kwa upande wa Hammer Q ambaye ametoka katika kundi hilo wiki chache zilizopita alikiri kuwa kuna siri katika kundi hilo lakini hakuwa tayari kuifichua.
Lakini alieleza kuwa siku akikutana na AT huenda wakazungumza na kukubaliana kuisema siri hiyo.
Siku tukikutana na AT…kwa sababu yeye mwenyewe ni mtu wa mishemishe na mimi mtu wa mishemishe kwa hiyo kama tukikutana hivi tunaweza tukaizungumza kama ikitokea tukakutana pamoja…tunaweza tukaisema hiyo siri.” Amesema Hammer Q.
Wasikilize hapa wakieleza kwa urefu:


Post a Comment

Previous Post Next Post