Hii ndio Video ya kundi la Sauti Sol ‘Nishike’ iliyofungiwa kuoneshwa na vituo vya TV Kenya

Sauti sol
Ule msumeno wa kuzifungia video za wasanii kutooneshwa katika vituo vya TV umelikumba kundi la Sauti Sol kutoka Kenya, ambao wiki hii wameachia video iliyoonekana kupokelewa vizuri na mashabiki wengi, toka ilipowekwa youtube April 29 hadi leo tayari imetazamwa mara 143,892.



Akiongea wakati wa tukio la tuzo za Mdundo jana jijini Nirobi, member wa kundi hilo Bien Aime alisema kuwa video ya ‘Nishike’ imefungiwa kuoneshwa na vituo vya TV vya Kenya na sababu walizopewa ni kuwa inachochea ngono.
Hiyo si video ya kwanza kufungiwa Kenya, video nyingine iliyowahi kufungiwa Kenya ni pamoja na ‘You guy’ ya P-Unit.
Source: Ghafla

Post a Comment

Previous Post Next Post