Hiki Ndicho Kilichomkasirisha Yaya Toure Manchester City

Screen Shot 2014-05-21 at 6.31.19 AMWakala wake anasema kama club hiyo isipompa heshima Yaya Toure anaweza kuondoka wakati wowote kwa sababu hakuna mchezaji yeyote au mtu yeyote anaependa kufanya kazi kwenye ofisi ambayo haimuheshimu ndio maana anaionya Manchester City imuombe msamaha.
May 13 2014 Yaya alitimiza umri wa miaka 31 hivyo alitegemea club yake ingempa heshima au kuipa nafasi siku yake ya kuzaliwa lakini badala yake ikachukuliwa poa tu, kitendo kilichomkasirisha Yaya na kuwamaind viongozi wa club hiyo.
Pamoja na kwamba hajawakasirikia wachezaji wenzake, unaambiwa walipokua kwenye ndege kuelekea Abu Dhabi kusherehekea ubingwa wao inadaiwa wachezaji wenzake walipendekeza muhudumu wa ndege ndio ampelekee Yaya keki ya birthday.

Screen Shot 2014-05-21 at 6.30.44 AM
Wakala wa Yaya anasema ‘Yaya amefanya mengi kwa ajili ya Manchester City, inasikitisha kwenye siku kama hii kuona hakuna kupewa mkono wa pongezi kutoka watu wanaofanya kazi sehemu moja, amekasirika kwa kweli… hii sio kawaida, hatutaki pesa wala zawadi bali attention, atleast tambua umuhimu wa hiyo siku kwa mchezaji mkubwa ndani ya club… hauwezi kuupata uhusiano mzuri kwa pesa au kuununua, inatakiwa wafanye hii kutoka moyoni’
Kwa kuongezea Yaya Toure aliandika kwenye page yake ya twitter kwamba maneno yote yaliyosemwa na Wakala wake ni ya kweli na kwamba yeye mwenyewe atafanya interview baada ya kombe la dunia kuzungumza kila kitu’

Screen Shot 2014-05-21 at 6.50.21 AM
Kwenye sentensi nyingine Wakala huyu wa Yaya Toure alipoulizwa kama Yaya ataendelea kubaki Manchester City baada ya kombe la dunia kumalizika, amejibu ‘sijui…. Yaya mwenyewe ataongea na Man City kisha tutafanya maamuzi baadae, ni club nyingi zinamtaka hivyo hakutakua na kazi ngumu kupata kazi sehemu mpya’

Post a Comment

Previous Post Next Post