Hivi Ndio Vikwazo Walivyovitaja Riyama na Wastara vya Filamu za Tanzania kupenya kimataifa


Waigizaji wa filamu nchini, Riyama na Wastara wamesema wasanii wa Tanzania wamekosa sauti moja jambo ambalo linachangia kuzorotesha ukuaji wa filamu za Tanzanuia. Wasanii hao waliopo nchini Uingereza kikazi walikuwa wakizungumza na BBC.
“Watu wengi wanasema sisi ni watengenezaji filamu local ,lakini zakwetu na za Kinaijeria hazina tofauti sana,kikubwa ambacho kinasababisha kuamua sisi kutengezeza filamu local ni kipato, kwasababu hata malipo yetu sisi na Wanaijeria ni vitu viwili tofauti, kwahiyo wao wanauwezo wa kuagiza vyombo vya production vyenye quality nzuri kwasababu wana uwezo wa kuilipa, akini pengine pesa kwangu mimi ya kuwalipa na kufanyia filamu yote wao ni ya kuagiza equipment ya kufanya movie moja, ndio maana sisi tunashindwa,” alisema Wastara.
Naye Riyama alisema:
“Wanasema umoja ni nguvu utengano ni udhaifu na katika tasnia yetu ya filamu Tanzania umoja kwetu ni haba sana, ubinafsi, kuna umimi, sio ile tufanye kitu kwaajili ya wote, kizazi cha leo,cha kesho na hata kijacho, kwasababu mimi naamini kidole kimoja hakivunji chawa, siku zote toka nimeingia kwenye tasnia ya filamu takriban miaka kumi na tano inafika,lakini tumekuwa tukililia umoja ,umoja lakini umekuwa ukiishia hewani.”

Post a Comment

أحدث أقدم