Msanii wa kundi na kampuni ya Weusi, Nick wa Pili ameweka wazi
kuwa siku za hivi karibuni itafahamika hatima ya Lord Eyes
aliyesimamishwa kutokana na kukiuka maadili na sheria za kundi.

Weusi
Nick aliweka wazi hilo alipokuwa akichat katika ukurasa wa Facebook
wa EATV alisema kuhusu hatima ya msaniii Lord Eyes ambae alisimamishwa
katika kundi hilo na kudai atarudishwa soon. “Lord Eyes soon atarudi
weusi maana sisi kama weusi kwa pamoja ni kampuni,hivyo weusi ni mtu 5
kama memorandam ya kampuni inavyo sema,” alisema.
Weusi walimsimamisha rapper huyo baada ya kutuhumia kuvunja kioo cha gari jijini Arusha na kuiba laptop.
إرسال تعليق