Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mkoa, Mary Moyo alilazimika kuahirisha kesi hiyo hadi Mei 14, mwaka huu.
Jana Shehe Ponda alifikishwa mahakamani hapo saa 3 asubuhi chini ya
ulinzi mkali wa Polisi. Wafuasi wake waliokuwepo mahakamani hapo,
walizuiwa nje ya uzio wa mahakama hiyo.
Hakimu Moyo anayesikiliza kesi hiyo, alitumia dakika tatu kufikia uamuzi
wa kuahirisha kesi hiyo. Aliufahamisha upande wa Wakili wa Serikali na
utetezi kuwa hakuwa na jalada halisi la kesi hiyo.
Jalada hilo limepelekwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa ombi la
Shehe Ponda la kutaka uamuzi wa mahakama hiyo, kupitiwa upya na Mahakama
ya juu.
Post a Comment