- Kinana awatembelea wafanyabiashara soko kuu Igunga
- Azungumza nao na kujua changamoto zao
- Asisitiza viongozi wengine kuwa karibu na wananchi na kuwasikiliza
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na mfanyabiashara katika soko
kuu la Igunga baada ya kumaliza mkutano wake kwenye kiwanja cha Sokoine
jana jioni tarehe 9 Mei 2014.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia tangawizi katika soko kuu la
Igunga ,Katibu Mkuu alipita sokoni hapo kuwasalimia wauzaji na
kuzungumza nao baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara kwenye kiwanja
cha Sokoine Igunga mjini jana tarehe 9 Mei 2014.
Mfanyabiashara
wa Soko la Igunga akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Igunga ndugu
Elibariki Kingu na kumuambia soko hilo linahitaji mitaro ya kupitisha
maji ya mvua sokoni hapo mbele ,wengine pichani ni Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
jana tarehe 9 Mei 2014.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akichagua Nanasi kwenye soko la Kuu la
Igunga mwingine pichani ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abrahman Kinana akikatiza katikati ya soko kuu la Igunga jana
jioni baada ya kumaliza mkutano wa hadhara katika kiwanja cha Sokoine.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi ya matango kutoka kwa akina
mama wafanyabiashara soko kuu la Igunga ,Katibu Mkuu alipita
kuwasalimia na kuzungumza na wafanyabiashara sokoni hapo.
إرسال تعليق