Madaktari
bingwa wa viungo na mgongo kutoka India, wanatarajia kuwasili nchini wiki hii
kwa ajili ya kuwachunguza na kutibu watu wenye maradhi hayo.
Taarifa
iliyotolewa na Mwenyekiti wa Hospitali ya Regency, Dk Rajni Kanabar
ilisema madaktari hao, wataendesha kambi ya siku mbili kuanzia Mei 17 mwaka
huu.
Iliwataja
wataalamu hao kuwa ni Dk Dipak Deva na Dk Ronak Desai, ambao ni wataalamu wa
mgongo na viungo. Mwingine ni Dk Hemang Baxi, ambaye ni mtaalamu wa vibofu vya
mkojo na saratani. Mtaalamu mwingine ni Dk Jignesh Patel na Dk Tarum Dave,
ambao ni wataalamu wa maradhi ya moyo.
Ilisema
kambi ya uchunguzi wa maradhi hayo, imeandaliwa kwa pamoja na Klabu ya Lions ya
Dar es Salaam na Hospitali ya Regency.
Taarifa
hiyo iliwataka watu wenye maradhi hayo, kutumia fursa hiyo kupata matibabu
kutoka kwa wataalamu hao.
“Ujio
wa wataalamu hawa ni fursa nzuri kwa watu wenye maradhi ya aina hii, kwani
Watanzania wengi hawawezi kumudu kwenda India kutibiwa, sasa watumie fursa hii
kuwaona madaktari hawa wakiwa hapa hapa nchini,” ilisema taarifa hiyo.
إرسال تعليق