Wafanyakazi
wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) wamegoma kufanya kazi
kwa kushinikiza kulipwa mishahara yao ya miezi mitatu.
Wafanyakazi
hao walianza mgomo huo juzi wakishinikiza uongozi wa mamlaka hiyo kuwalipa
mishahara yao ya kuanzia mwezi Februari mpaka Aprili, mwaka huu na pia madai ya
mamlaka hiyo kuzembea katika usimamizi wa vitendea kazi.
Jana
safari za kwenda Kapili Mposhi nchini Zambia na kuja Dar es Salaam zilifutwa
kutokana na mgomo huo ambao pia umehusisha treni inayofanya safari zake kutoka
kituo cha Tazara mpaka Mwakanga.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyanyakazi wa Reli nchini (Trawu), Dar es Salaam yasin Mleke
alisema, wafanyakazi wamekuwa wakifanya kazi bila malipo yao hali inayowafanya
kuishi katika hali ngumu.
"Wafanyakazi
wamekuwa na njaa tangu Februari. Wananusirika kwa kukopa chakula katika maduka
mbalimbali na baadhi yao tayari wameshaenda kushitakiwa katika ofisi za serikali
za mitaa kujibu mashtaka kwa kutolipa madeni," alisema Mleke.
Aidha,
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tazara, Conrad Simuchile alinakunusha madai
ya kuwepo kwa uzembe na kusema, "Katika miezi 12 iliyopita Tazara kwa
wastani ilikpata mapato ya karibu dola za Marekani milioni 2.5.
"Kati
ya kiasi hicho, angalau dola za Marekani milioni 1.4 huenda kwa wafanyakazi kwa
ajili ya mishahara ya kila mwezi, mafuta ya kuendesha injini, matengenezo
ya madaraja na mahitaji mengine, " alisema Simuchile.
Alisema
katika kipindi cha mwezi Januari na Machi tani 4,000 za mizigo zilizafirishwa
kwa wastani kwa mwezi na kuzalisha kiasi cha dola za Marekani 400,000, kiasi
ambacho hakitoshi hata kulipa theluthi moja ya wafanyakazi hao.
Katibu
wa Trawu tawi la Dar es Salaam Waziri Mwenevyale aliishauri menejimenti ya
Tazara kuacha ubaguzi linapokuja suala la usafirishaji wa mizigo..
Alisema
ni wakati wa Tazara kushiriki katika biashara kubwa na kuachana na siasa zisizo
na manufaa. "Ni ajabu kwamba hata baadhi ya maamuzi eti yanatolewa na
mikoa, utawala ni kama umetekwa nyara na Makao Makuu na kama mikataba
inavyoelekeza katika sheria ya Tazara ya mwaka 1995," alisema.
Akizungumza
na gazeti hili mmoja wa abiria aliyekuwa akisafiri kuelekea Mbeya
aliyejitambulisha kwa jina la Amina Said alisema kuwa mgomo huo kwa kiasi
kikubwa umewagharimu kutokana na wengi wao kutoka mbali na wana watoto wadogo.
"Hata
wewe huyu mtoto mdogo niliyenaye hapa anapata tabu kwa sababu kwanza baridi,
kwa hiyo tunaomba tuangaliziwe namba nyingine ya kusaidiwa kuweza kufika
tunapoenda na hasa kwa kuangalia tunatoka mikoani," alisema.
إرسال تعليق