Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande, amesema Mahakama imejipanga kuondoa
tatizo la mlundikano wa mashauri ya muda mrefu ndani ya miezi18 ijayo.
Kauli
hiyo aliitoa jana katika ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Mahakama uliofanyika
mjini hapa.
Alisema
mashauri hayo yako mahakamani kwa zaidi ya miaka miwili na kuendelea na
lengo
ni kuondoa tatizo hilo ambalo limekuwa likilalamikiwa na wananchi wengi.
Jaji
Chande alisema Mahakama imeamua kufanya kazi kwa malengo na vipimo kwa kumaliza
mashauri kwa wakati.
Alisema
sasa kila Mahakama imeainisha kesi zote za muda mrefu za zaidi ya miaka miwili;
“tunataka miezi 18 ijayo kesi ziondoke na kutolewa hukumu.”
Jaji
Chande alisema Mahakama imejipanga kuhakikisha
kuna kuwa na upatikanaji wa taarifa kwa wakati na taarifa hizo zitakuwa zikikusanywa kila baada
ya wiki mbili.
Alisema
Mahakama imejipanga kuweka usimamizi na ufuatiliaji kwa mwaka ujao kuanzia
ngazi ya chini hadi ya juu, ambapo kabla ya Bajeti ijayo, mikoa takribani nane itapatiwa
magari kwa ajili ya kufanya ukaguzi katika mahakama mbalimbali kuangalia
mienendo ya mashauri.
“Mafanikio ni mengi lakini ni lazima tuwe na
malengo katika kuboresha utendaji kazi wa kila siku ili kuhakikisha hatua
inapigwa,” alisema.
إرسال تعليق