Fedha
zinazopelekwa Zanzibar kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya
kusaidia shughuli mbalimbali za kibajeti, kiuchumi na kijamii, zimewekwa
wazi ambapo miongoni mwake zipo zinazotokana na Malipo ya Kodi ya Mishahara
(Paye).
Wakati
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Samia Suluhu Hassan
aliwasilisha taarifa hiyo jana bungeni, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba,
Sheria na Utawala, ilisema kutofahamika kwa fedha zinazopelekwa Zanzibar
kutoka Serikali ya Muungano, kunachangia baadhi ya watu kubeza
Muungano.
Waziri
Samia alitoa taarifa hiyo wakati wa kuwasilisha
makadirio ya Bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2014/15.
Alisema
kuanzia Julai Mosi, 2013 hadi Machi 31 mwaka huu, Sh bilioni 15.75 za Paye
zimemepokewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Fedha
hizo za Paye kwa mujibu wa Waziri, ni matokeo ya makubaliano kati mawaziri wa
SMZ na wa Muungano baada ya kuwepo madai ya Zanzibar kutaka kupata fungu
kutokana na mapato hayo kwa wafanyakazi wa taasisi za Muungano wanaofanya kazi
Zanzibar.
“Hata
hivyo marekebisho ya kisheria hususani Sheria ya Kodi ya Mapato (Paye) yanahitajika ili kuweka utaratibu wa
wazi,” alisema Samia.
Licha
ya Paye, gawio lingine kwa SMZ ni linalojumuisha asilimia 4.5 ya misaada ya
kibajeti. Alisema hadi Machi mwaka huu, SMZ imepata msaada wa kibajeti wa Sh bilioni
27.19 kati ya Sh bilioni 32.62 zilizoidhinishwa na Bunge kwa mwaka wa fedha
2013/14.
Aidha
katika kipindi cha kuanzia, fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo zilizopelekwa
Zanzibar ni Sh bilioni 1.24. Vile vile Serikali ya Muungano ilichangia Sh
milioni 600 kwenda SMZ kwa ajili ya kufanikisha maadhimisho ya miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Vile
vile Waziri alisema katika kipindi hiki, masuala ya kijamii yameratibiwa na
kunufaisha wananchi wa pande zote za Muungano.
“Serikali
zetu kwa ushirikiano zimeendelea kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali kwa
ajili ya maendeleo ya wananchi wake.”
Alitaja
miradi hiyo inayofadhiliwa na Serikali kwa kushirikiana na washirika wa
maendeleo. Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii Tanzania (Tasaf), Mradi wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP), Mradi wa
Maendeleo ya Mifugo (ASDP-L) na Millennium Challenge Account Tanzania
(MCA).
Katika
mwaka wa fedha 2014/15, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano imeomba Bunge
liidhinishe Sh bilioni 5.7 kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Kiasi hicho
kinajumuisha fedha za mishahara Sh milioni 879.5 na fedha za matumizi mengineyo
Sh bilioni 4.84.
إرسال تعليق