Man U yalowa kwa Sunderland

Danny Welbeck akijaribu kuwatoka wachezaji wa Sunderland
Kaimu Meneja wa Manchester United Ryan Giggs amepata pigo la kwanza baada ya timu yake kupokea kichapo cha goli moja kutoka kwa Sunderland siku ya Jumamosi.
Sebastian Larsson wa Sunderland ndiye aliyezima ndoto za ushindi za Manchester United katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford baada ya kupachika goli zuri katika dakika ya 29 kipindi cha kwanza.
Sunderland ambayo ilikuwa inapigania kuepuka kushuka daraja ilionekana kutawala mchezo ambao Emanuel Giaccherini na Fabio Borin walikosa magoli baada mashuti yao kugonga mwamba.
Kipindi cha pili Manchester walikuja juu na kujaribu kusawazisha goli lakini wakakosa umakini wa umaliziaji.
Kwa matokeo hayo Manchester United inaendelea kubaki nafasi ya saba na pointi 60 huku Sunderland wakijihakikishia kutoshuka daraja baada ya kujikusanyia point 35 huku wakiwa wamebakiza michezo miwili.

Post a Comment

أحدث أقدم