
United wamekubaliana na Bayern Munich kuuziana Toni Kroos (katikati).
MANCHESTER United  amekubaliana dili la kumsajili kiungo wa Bayern Munich, 
Toni Kroos na sasa wanajipanga kuiwinda saidi ya mchezaji mwenzake, Mholanzi Arjen Robben.
Kross 
alikubaliana na ofa ya paundi milioni 20 na aliyekuwa kocha wa 
Manchester United, David Moyes na mrithi wake ambaye aliyewahi kuwa 
kocha wa Bayern Munich, Louis Van Gaal amebariki dili hilo kuendelea.
Kroos, 
24, aling`ara wakati wa utawala wa Van Gaal katika klabu ya  Bayern na 
bado anahitaji kufanya kazi na kocha  wake wa zamani.
 Yupo kwenye rada: United kwasasa wapo katika mawindo ya kumnasa nyota wa Bayern,  Arjen Robben
Yupo kwenye rada: United kwasasa wapo katika mawindo ya kumnasa nyota wa Bayern,  Arjen Robben
Tabasamu tu: Kocha wa Uholanzi, Louis Van Gaal  akitasamu katika mazoezi ya timu yake mjini Lagos nchini Ureno.
Robben ni
 mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Van Gaal wakati akiwa Bayern kwa ada 
ya uhamisho wa paundi milioni 20 kutokea klabu ya Real Madrid mwaka 
2009.
Siku za 
karibuni winga huyo mwenye miaka 20 alisaini mkataba wa miaka mitatu na 
Bayern, lakini haimvunji moyo Van Gaal ambaye atafanya kazi na Robben 
katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Inafahamika
 kuwa United wamekubaliana dili la paundi milioni 27 ili kuinasa saini 
ya beki wa kushoto wa Southampton,  Luke Shaw na beki wa kati wa 
Borussia Dortmund,  Mats Hummels yupo katika mipango ya Van Gaal.
Post a Comment