Aidha,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeshafanya utafiti mkoani Kagera,
Morogoro na Kigoma na kuthibitisha kuwa haijaathirika na ugonjwa
huo.
Wakati
ugonjwa huu umetajwa kukumba zaidi ukanda wa joto, Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii imeandaa mpango kwa kushirikiana na sekta mbalimbali kuudhibiti.
Taarifa
hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk
Stephen Kebwe ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Kiti cha Spika baada ya
Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile kuomba mwongozo wa spika juzi, kutaka
Serikali kutoa taarifa rasmi bungeni.
Dk
Kebwe ambaye alisema Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kukabili
ugonjwa huu kadri itakavyohitajika, alihimiza uvaaji wa nguo ndefu na zenye
mikono mirefu, hususani katika maeneo ambayo ugonjwa huu umeripotiwa.
Alisema
timu ya taifa ya maafa, inayoshirikisha halmashauri za Kinondoni, Temeke na
Ilala inaendelea kukutana kila wiki.
Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii imeshafanya utafiti katika mikoa ya Kagera, Morogoro
na Kigoma na kuthibitisha kuwa haijaathirika na mkoa huo.
Ugonjwa
huo unaotokana na kirusi, kinachosambazwa na mbu aina ya Aedes, idadi ya
wagonjwa tangu Januari mwaka huu hadi sasa ni 458 na vifo vitatu.
Dalili
za ugonjwa huo ni homa, kuumwa kichwa, maumivu ya viungo na uchovu huku wakati
mwingine, dalili zake zikifanana na za malaria.
Post a Comment