Katibu
Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Unguja
waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo
la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar.
Maelfu ya Wananchi wakishangilia huku
wakionyesha ishara ya serikali mbili, wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa
na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye Viwanja vya Kibandamaiti mjini
Zanzibar jioni ya leo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd
akiwasalimia wananchi wa Unguja waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa
hadhara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika jioni ya leo kwenye
Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar.
Mke
wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar,Hayati Aman Karume,Mama Fatma Karume
akiongea kwa msisitizo mkubwa huku akiwataka Wazanzibar kuacha kabisa
kuuchezea Muungano kwa kuwafuata watu wanaoupotosha.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akimpongeza Mke wa Rais wa Kwanza
wa Zanzibar,Hayati Aman Karume,Mama Fatma Karume mara baada ya
kuzungumza na wazanzibar jioni ya leo waliofurika kwa wingi kwenye
Uwanja wa Demokrasia ,Kibada Maiti mjini Unguja.
Katibu
wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akiwaeleza wananchi wa
Unguja kuhusu umoja ulioanzishwa wa baadhi ya vyama vya siasa na malengo ya
umoja huo,wakati wa Mkutano wa Hadhara wa Chama cha
Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo
eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar.
Mbunge
wa Viti Maalum CCM,Mh. Ummy Mwalimu akiwahutubiwa wananchi wa Zanzibar
kupitia Mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Uwanja wa
Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar jioni ya
leo,ambapo amewataka Wazanzibari kutohadaishwa na UKAWA kuhusu swala la
muundo wa Serikali katika mchakato wa Katiba.
Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini,Mh. Emmanuel Nchimbi akinukuu sehemu ya
maandishi yaliopo kwenye kitabu cha Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad wakati wa Mkutano wa hadhara wa CCM
uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la
Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar.
إرسال تعليق