WANACHAMA wa Kundi la
Mpira Pesa la Simba, wamefunguka kuwa, anayefaa kuwa rais wa klabu hiyo
kwa miaka minne ijayo ni Hassan Dalali kwa kuwa ni mtu mwenye hekima na
busara.
Dalali aliwahi kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo kabla ya Ismail Aden Rage lakini alipigwa zengwe katika uchaguzi uliopita kutokana na kukosa cheti cha kidato cha nne na sasa yupo ‘skuli’ anaendelea kula kitabu apate cheti hicho.

Simba inatarajia kufanya uchaguzi mkuu Juni 29, mwaka huu kwa nafasi
mbalimbali za urais, makamu wa wa rais na wajumbe wa kamati ya utendaji
watakaoiongoza klabu hiyo kwa kipindi cha miaka minne.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Mwenyekiti wa Tawi la Mpira Pesa lililopo Magomeni jijini Dar, Ustadhi Masud, alisema wanamchukulia Dalali kama Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokana na kufanikiwa kuondoa makundi ndani ya klabu hiyo tangu alipopata madaraka mwaka 2006.

“Simba kwa sasa inahitaji kiongozi mwenye hekima na busara tofauti na
kiongozi aliyepita Ismail Aden Rage ambaye anaonekana kujisifu yeye na
kuwatukana watu, jambo hilo halikuwepo katika uongozi wa Dalali ambaye
amekuwa na sifa zote za kuwa kiongozi.
“Kiongozi anayetakiwa kuongoza awe msikivu kwa kusikiliza fikra za
kila mtu mwenye uwezo na asiye na uwezo kwani Simba ni ya watu
tofautitofauti, Dalali ni mtu anayefaa kuongoza tena Simba kwani
tunamchukulia kama Nyerere, japokuwa uchukuaji wa fomu ni mapendekezo ya
mtu binafsi, hatuwezi kumlazimisha lakini iwapo atachukua basi huyo
ndiye tunayemhitaji.
“Alikuja Simba mwaka 2006 na kukuta makundi na alifanikiwa kuyaondoa.
Pia alifanikiwa kutwaa ubingwa bila kufungwa na kutoa sare mbili tu,
vilevile hana kashfa yoyote ya kuihujumu timu. Na kama yeye hatagombea,
mtu anayetakiwa kugombea awe mwenye sifa kama zake,” alisema Masud.
Post a Comment