Msanii AMANI toka Kenya, adatishwa na ‘ZEGE’ la Kibongo

20140503-144920.jpg
Katika mtandao wa kijamii Twitter, mwanadada msanii toka nchini Kenya akiwa jijini Dar Es Salaam kwa sasa kwa ajili ya ‘Kilimanjaro Music Awards 2014′ KTMA ambayo yanafanyika siku ya LEO, muda si mrefu aliandika…
“I like the food in Tz…trying to resist the temptation to have some ‘zege’ a.k.a. Chips mayai…woooiii” @AmaniMusician
20140503-144647.jpg
Zege” ni chakula maarufu sana nchini Tanzania hasa jijini Dar Es Salaam ambacho kuanzia miaka ya 90 ndio vibanda vingi sana vya ‘Chips’ vilijengwa maeneo mbali mbali na kusabisha kuwa kama ni “Junk Food” ya kitanzania ukilinganisha na ‘Burger’ ambazo zilianza kuingia nchini humo kuanzia miaka ya mwishoni mwa 90 na kuchanganya zaidi miaka ya mwanzoni mwa 2000 katika sehemu kama mjini kama, Steers.
Chips Mayai Aka ‘Zege’ kawaida yake huenda lenyewe ‘KAVU’ (Chips Kavu) au linaweza likaja na MISHKAKI au KUKU (Chicken), ambapo pia neno “CHIPS KUKU” (Chicken Chips) likawa maarufu sana jijini Dar Es Salaam Miaka hiyo ya nyuma, kuweza kuimbwa sana kwenye chimbuko la muziki wa kizazi kipya ambao ndio unaongoza kupigwa kwenye radio nyingi sana za East Africa. “Chips Kuku” linatumika mpaka sasa kwenye Local Hotels na Restaurants MENU. CHIPS MAYAI inajulikana kwa majina mengine mengi au kama watanzania waliokuwa wakiishi nchini Uingereza miaka ya kuanzia 2005 ‘Northampton House Building’ katika Mji wa Northampton nje kidogo ya mji mkuu wa London, wao walikua wanatambulisha chakula hicho kama “Kama Kawa”.
Karibu Tanzania, ukifika tafuta “Zege” halafu utaniambi Balaa lake.
CHIPS KUKU
20140503-144811.jpg
CHIPS MISHKAKI
20140503-144854.jpg

Post a Comment

أحدث أقدم