Mayweather amchapa Maidana kwa ‘SHIDA’ sana - BOXING

LAS VEGAS — Hii ni moja kati ya Ushindi wa $32 million Floyd Mayweather Jr. Ametengeneza kwa jasho zito sana pesa hiyo, baada ya Marcos Maidana kumdindishia “Champion” huyo kwenye “Tough 12 Round” kabla hajashindwa kwa maamuzi yaliyo ya wengi kutoka kwa majaji “majority decision” katika mchezo uliomalizika muda si mrefu ndani MGM Grand Hotel mjini Las VEGAS Nevada. Mayweather ameemdelea kuwa “Champion” lakini kwa walioangalia pambano wanaweza kukubaliana na mimi kabisa kuwa mchezo haukuwa rahisi wala wa kitoto kuweza kujishindia kirahisi rahisi tu sababu ‘Maidana’ alimkamia na kumkakamalia tokea Kengele ya “1st Round” na kumpa bingwa huyo mchezo mgumu sana ambao hajawahi kuupata katika miaka 16 ya “Professional Boxing Career”
“It was a tough, competitive fight, I normally like to go out there and box and move. But he put pressure on me. I wanted to give the fans what they wanted to see so I stood and fought him.” – Floyd Mayweather Said
Maidana aliinua mikono juu kwa kuonyesha ushindi baada ya kengele ya mwisho kulia kuonyesha ushindi huku akimuangalia mpinzani wake akiwa ametulia kwenye kona bila ya kuonyesha uhakika wa ushindi kabla Maywether hajatangazwa mshindi kwa kura za wengi.
“I think I won the fight, He didn’t fight like a man.” – Maidana Said.
“Compubox” inaonyesha kuwa Mayweather ameshusha “Punch 230″ ambazo zilimpata Maidana kati ya 426 alizorusha na alishushiwa “Punch 221″ kati ya 858 alizotupiwa kutoka kwa Maidana. Na hii imevunja record ya Mayweather kupigwa punch nyingi kuliko alizopigwa na Boxer yoyote katika zaidi ya michezo 38 aliyowahi kuicheza mwana masumbwi huyo.
“I couldn’t see for two rounds after the head butt,” Mayweather said. “After I could see again it didn’t both me. That’s what champions do, they survive and adjust.”
Maidana alisema mwanzoni kabisa kuwa, atapigana na Mayweather kama anavyopigana na mabondia wengine kuacha unaarufu wake au ubingwa alionao na aliweza kufanya hivyo baada ya kuwa anamfata kila anapoenda na kumtupia masumbwi pamoja na kuyakwepa ila hakuacha kumfata, hiyo inasababisha Maidana kutupa masumwi zaidi ya nusu ambayo Mayweather aliyatupa.
“He never hurt me with a punch,” Maidana said. “He wasn’t that tough, I thought I won.”
Maidana alilalamika kuwa alilazimishwa kucheza na Gloves asizotaka kutumia na alisema kama angetumia Gloves zake alizopanga sasa hivi tungekua tunaongelea “Knock Out” sababu ameona ji jinsi gani angeweza kumchapa mpinzani wake huyo.
“If I would have had my gloves I would have knocked him out,” Maidana said. “They took away my advantage.”
Mayweather alionekana kuchanganyikiwa kwenye Round za mwanzo sababu alishindwa kuzoea mvua ya ngumi iliyokuwa inammiminikia kutoka kwa Maidana mpaka round za kati kati ndio akaonekana kuingia na kuweza kucheza na “Rhythm” aliyokuwa nayo Maidana, baada ya kuwa anamchapa Maidana kwenye mwilimi kwa ngumi za kushoto na kulia alikua anamdondoshea kichwani.
Mayweather alisema hababaishwi na mwana masumbwi huyo, na akasema kuwa kama Fans wanataka kuona anaweza kumuadhibu vipi Maidana, yeye yupo tayari kuzipiga tena na mwana masumbwi huyo kumuonyesha kuwa nani ni Champion wa ukweli.
“If the fans want to see it again, let’s do it again,” Mayweather said.

Post a Comment

أحدث أقدم