Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwauliza baadhi ya wanafunzi waliofika
kwenye uzinduzi wa wiki ya elimu uliofanyika katika uwanja wa jamhuri
ambao unafaika kitaifa mkoani Dodoma, kama wana uelewa kuhusu neno Big
results now akiwa na maana ya matokeo makubwa sasa kielimu.
Katibu wa Chama cha walimu Dodoma Gerge Palapala akimfafanulia jambo
Waziri Mkuu Mzengo Pinda alipotembelea Banda la chama hicho lililopo
katika viwanja vya Jamhuri kwa ajili ya maonyesho ya elimu yanayofanyika kwa wiki moja mjini Humo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia Tufe lenye mfano wa Ramani ya Dunia
ambalo ni maarumu kwa kufundishia wanafunzi wenye ulemavu wa kuona
wanaosoma katika shule Iliyopo Bwigili Wilayani chamwino, alipokuwa
akikagua mabanda ya maonyesho kwenye uzinduzi wa wiki ya elimu
inayofanyika kitaifa Dodoma.
Mratibu wa taifa wa masomo ya Sayansi, Hisabati na Tehama DKT Elia
Kibga akimufafanulia jambo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipotembelea Banda
la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakati wa uzinduzi wa wiki ya
Elimu inayofanyika kiataifa Dodoma
Mwanafunzi Mandela Mazengo (9) mwenye ulemavu wa macho akimuandikia neno
kwa kutumia kifaa maalum kinachoandika maandishi yanayoweza kusomwa na
wasioona kwa njia ya vidole wakati alipotembelea Banda la shule ya
wasioona ya Bwigili Iliyop Chamwino Dodoma, Pinda alifika kuzindua wiki ya elimu iliyoanza Aprl 3,2014 yanayofanyika kitaifa mkoani humo
Wanafunzi wakiwa katika jukwaa la uwanja wa jamhuri wakifuatilia
matukio mbali mbali wakati wa uzinduzi wa wiki ya Elimu uliofanyika
Dodoma ambapo maonyosho hayo yanafanyikia kitaifa. Picha na John Banda
إرسال تعليق