

Dj stone alisema kuwa msanii Prezzo na marafiki zake walimpiga sana na baada ya kushindwa kumlipa Prezzo pesa ya mafuta ya gari yake, Alisema “Niliandaa show yangu iliokwenda na sambamba na Bigbrother tour iliofanyika hapa nchini eneo la Kitengela, Nilimlipa Prezzo Sh40,000 kabla ya show na baada ya show nlimlipa kiasi kilichobaki, kulingana na makubaliano yetu.. Prezzo alitaka nimlipe tena kiasi cha Sh5,000 kwaajili ya mafuta ya gari yake”

“Walinipiga kichwa, tumbo na sehem zingine za mwili na kunitishia kuniua endapo nitashtaki kokote au kutoa taarifa polisi.”
Prezzo alikanusha na kusema hakuna walichomfanya Dj stone na baadala yake walikua nae karibu ili awalipe kiasi cha pesa yao baada ya kumaliza show hiyo. Pamoja na yote hayo Dj stone alitupeleka club, alikodai kuwa binamu yake anafanya kazi sehemu hiyo kama Dj.
Post a Comment