Mwanaume
mmoja Mtanzania amekamwata katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta
Nairobi Kenya akiwa amebeba dawa za kulevya akiwa njiani kuelekea
Antananarivo ambapo mzigo huo ulitokea Tanga kisha ukapita Mombasa na
baadae kwa ndege mpaka Nairobi.Mzigo wenyewe ni wa cocaine na Heroin
ambazo zote zina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 24 za Kitanzania
na dawa hizo alikua ameziingiza katika njia ya haja kubwa.Mkuu
wa kitengo cha CID katika uwanja huo Joseph Ngisa amesema mshukiwa
alikamatwa JKIA na akawekwa kwenye chumba cha uchunguzi na baadae akatoa
tembe za cocain na tembe za Heroin na tayari ameshapelekwa Mahakamani.
Mwezi
March mwaka huu watanzania wanne walikamatwa katika uwanja huohuo
walipopatikana na heroin yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 75
za Kitanzania na wote walifikishwa mahakamani na kukiri kosa.
Wanawake
watatu na mwanaume mmoja kila mmoja akishtakiwa kando kwa kosa la
kusafirisha dawa za kulevya na walikua wameingia Kenya kupitia Namanga
na walikamtwa wakiwa njiani kuelekea Hong Kong.
Kuanzia
March 2014 mpaka leo hii May ni jumla ya Watanzania watano wamekamatwa
kwenye kiwanja cha ndege Nairobi wakiwa kwenye pilika za kusafirisha
dawa za kulevya kwenda kwenye mataifa mengine.
إرسال تعليق