Rihanna ameimwaga label yake ya muda mrefu ya Def Jam Records na
kujiunga na label inayoongozwa na Shawn Carter aka Jay Z, Roc Nation,
jarida la Complex limeripoti.
Pamoja na Riri (26) kuachana na Def Jam lakini album yake ijayo
ambayo itakuwa inafuata baada ya ‘Unapologetic’ ya mwaka 2012,
itaendelea kusambazwa na label hiyo.
Awali Jay Z ndiye aliyemsaini Rihanna kipindi alipokuwa bado ni rais
wa Def Jam kabla hajajiondoa mwaka 2009 na kuanzisha Roc Nation, lakini
uhusiano wao wa kikazi uliendelea kama kawaida.
إرسال تعليق