Rihanna, Ndani ya Black Bold ‘MABUTU’ na ‘Vampy Lips’ kwenye iHeart Music Awards.

20140502-084521.jpg
Rihanna siku ya tarehe 1 May alishangaza watu kwa style ya uvaaji aliyoingia nayo katika “iHeartRadio Music Awards” ambayo ilifanyika ndani ‘Shrine Auditorium – Los Angeles’, Rihanna aliingia na nywele nyeusiiii na Lip stick rangi hiyo hiyo ambayo ilifanya kila mtu kumuangalia yeye sababu alikua amevaa kama Gypsy. Muonekano huo sio kwamba ulishangaza na watu kumuona kitu cha ajabu hapana, kila mtu alisifia muonekano huo sababu kwa kifupi mwanadada huyo alipendeza.
Kwenye mtandao wa kijamii Twitter, mwanamitindo kutoka nchini Tanzania ambae anafanya kazi zake nchini Marekani ‘Flaviana Matata’ aliandika “She is a Risk Taker, I Lover Her” na kuweka picha ya mwanadada huyo na hii ni kutokana na uvaaji huo wa Rihanna ambao mpaka mtu uige lazima uwe na moyo maana risk ya kuwa “Kituko” ni kubwa sana.
Rihanna ambae ana umri wa miaka 26 tu na kuwa na mafanikio makubwa sana duniani, katika awards hizo alifanikiwa kuchukua award nne ikiwemo award kubwa ya “BEST ARTIST OF THE YEAR”.
20140502-084447.jpg

Post a Comment

أحدث أقدم