Ruvu Shooting yawatema sita kama Azam vile

Kikosi cha Ruvu kitakachopanguliwa wachezaji sita kutokana na pendekezo la kocha Tom Olaba
KOCHA mkuu wa Ruvu Shooting, Tom Olaba amependekeza wachezaji sita watemwe katika kikosi chake kitakachoshirikishi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao kutokana na utovu wa nidhamu.
Msemaji wa timu hiyo, Masau Bwire, aliiambia Hisia za Mwananchi kuwa, kocha Olaba katika ripoti yake ya msimu wa 2013/14 wa ligi hiyo, amependekeza wachezaji sita watemwe kutokana na utovu wa nidhamu na kushuka kwa kiwango cha soka.

Bwire hakuwa tayari kuweka wazi majina ya wachezaji hao hata hivyo. 
“Tutawataja muda ukifika,”amesema Bwire huku rungu hilo likionekana wazi litawakumba wachezaji waliotoroka kambini na kukimbilia Oman kwa ajili ya kufanya majaribio na wale waliotoroka kambini wakati timu ya 'maafande' hao wa Pwani ikijiandaa na mechi iliyopita dhidi ya Azam FC.
Aidha, katika mikakati ya kukisuka upya kikosi chao cha U-20 na timu ya wakubwa, uongozi wa umesema kutakuwa na majaribio ya wachezaji kati ya Mei 15 na 28 kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Mlandizi, Pwani.

“Mwenyekiti wa klabu, Kanali Nguge ameomba yeyote mwenye uwezo wa kucheza mpira, umri stahiki wa mpira, umbo na nidhamu kutoka sehemu yoyote nchini aje kushiriki majaribio hayo,” amesema Bwire.

Post a Comment

أحدث أقدم