KAMPUNI ya Samsung inayotengeneza
vifaa mbalimbali vya elektroniki imeamriwa kuilipa kampuni ya Apple dola za
Marekani milioni 119.6m (£71m) kwa kutumia ugunduzi wake bila ruksa.
Hukumu hiyoi ilitolewa juzi katika
mahakama moja ya California iliyoketi mjini San Jose.
Hukumu hiyo inatokana na shauri
la Apple ambalo limefanyika kwa karibu
mwezi mzima akituhumu Samsung kwa kukiuka sheria za haki miliki kwenye simu
zake za kisasa zenye shughuli nyingi( smartphone).
Pia
katika shauri hilo Apple nayo
ilionekana kukiuka haki miliki na kutakiwa kuilipa Samsung dola za Marekani 158,000.
Apple katika shauri lake iliitaka
ilipwe dola za Marekani bilioni 2.2 akituhumu Samsung kunakiri haki miliki zake
tano kwenye simu zake za kisasa.
Samsung ilikanusha na kuidai Apple dola za Marekani milioni 6 kwa
kunakiri haki miliki zake mbili katika simu yake ya kisasa kwenye kamera na
usafirishaji wa video.
Miaka miwili iliyopita jopo la
majaji liliagiza Samsung kuilipa Apple dola za Marekaniu milioni 930 baada ya
kuiona nah atria ya kurtumnia teknbolojia ya Apple.
Samsung mpaka leo imekata rufaa
kuhusu amri hiyo.
إرسال تعليق