Tukiwa tunaelekea kwenye
kilele cha sherehe zifanyikazo kila mwaka nchini Tabzania huko pande za
visiwani Zanzibar ikiwa hushirikisha wasanii wengi sana wanaotokea pande
za mashariki mwa afrika, Mwanamuziki Mkongwe wa Reggae Tanzania
Jhikoman akiwa na Afrikabisa Band atakuwa ni mmoja kati ya wasanii
wataofanya maonyesho Live ndani ya “Sauti Za Busara Music Festival
2014″. Huyu ni Mmoja kati ya wanamuziki wakubwa wa Muziki wa Reggae
hapa nyumbani Tanzania pamoja na Afrika Mashariki akiwa ameanza
kujulikana na kazi zake za muziki miaka ya 90 mwanzoni na hiyo ni zaidi
ya miaka 20 akiwa anasakata gurudumu la muziki hapa nchini na nje ya
nchi. Kwa sasa Jhikoman yupo katika Ziara yake ya Ulaya kufanya
Maonyesho katika Nchi za mbali mbali kabla ya kurusi nchini kwa ajili ya
maonyesho hayo.
إرسال تعليق