SERIKALI
imetoa maagizo kwa Chama Cha Hatimiliki Tanzania (COSOTA) kukutana na Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) kuangalia namna ya kuboresha stika zinazobandikwa
katika kazi za wasanii.
Naibu
Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwigulu Nchemba alitoa kauli hiyo bungeni jana
ambapo alitaka COSOTA na TRA kukutana ndani ya siku tano kuangalia
namna ya kuboresha stika zinazobandikwa katika kazi za wasanii ili badala
ya kutumika kukusanya ushuru peke yake zitumike pia kulinda kazi za wasanii hao
.
Pia
alisema kwa kazi zote zitakazokuwa zinauzwa bila stika au kwa kazi
zitakazobandikwa stika zisizo halali wachukuliwe hatua mara moja.
Mwigulu
alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Martha Mlata
(CCM) ambaye alisema stika ambazo zinatumika kulinda kazi za
wasanii hazisaidii badala yake zinawasaidia TRA peke yake kukusanya mapato
Aidha
akiuliza swali la nyongeza, Mbunge wa Kasulu, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi)
alisema kumekuwa na makampuni ambayo yananyonya wasanii na serikali ina kauli
gani katika hilo.
“makampuni
mengine bado yananyonya wasanii licha ya serikali kuanziish utamaduni wa kuweka
stempu kwenye kazi za wasanii lakini kazi zisizo na stempu bado zinahujumiwa
kwa nini msijifunze kutoka Nchini Uganda ambapo wamefanikiwa katika kulinda
kazi za wasanii? ” alihoji Mkosamali.
Akijibu
swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, vijana utamaduni na Michezo Juma Nkamia
alisema kuna taarifa kuwa kazi za wasanii zinazgaa mitaani na serikali
inachukua hatua kwa kushirikiana na wadau katika kuondoa kazi hizo.
“Kama
Uganda wamefanikiwa katika hili tuko tayari kwenda kujifunza” alisema
Awali
katika swali la msingi la Mbunge wa Kasulu Mjini, Agripina Buyogera
(NCCR-Mageuzi) alitaka kujua lini Serikali itawatambua wasanii kisheria
ili kulinda kazi zao ikiwemo kutunga sheria nzuri nzuri kulinda haki za
wasanii.
Akijibu
swali hilo, Nkamia alisema Serikali inawatambua wasanii wa filamu na muziki
pamoja na tasinia nyingine za sekta ya filamu.
Aidha,
alisema Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ipo katika hatua za maamuzi
Serikalini.
Source: Sifa Lubasi, habariLeo,BungeniDodoma
Post a Comment