Matukio
ya kuuawa kwa watu wenye ulemavu wa Ngozi (Albino) yamezuka upya mkoani
Simyu, ambapo mwanamke mmoja Mughu Lugata (40) mwenye ulemavu wa ngozi
(Albino) ameuawa kinyama kwa kukatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana
pamoja na kutoweka na baadhi ya viungo vyake.
Tukio
hilo lililotokea katika kitongoji cha chalala kijiji cha Gasuma kata ya
Nkololo wilayani Bariadi Mkoani hapa, marehemu alikatwa mguu wake wa
kushoto sehemu ya goti, vidole 2 mkono wa kushoto pamoja ukucha wa
kidole gumba , ambapo wahusika walitoweka na viungo hivyo.
Akitoa
taarifa mbele za waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa polisi
mkoani hapa Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo limetokea jana
majira ya saa 12 usiku hadi saa moja asubuhi,wakati marehemu akiwa
nyumbani kwake.
“marehemu
aliuawa na kiungo chake cha mguu wa kushoto kuchukuliwa kwa kukatwa
sehemu ya goti, vidole 2 vya mkono wa kushoto ambavyo ni kidole cha 3 na
4,kukatwa na kuchuliwa na ukucha wa kidole gumba cha mkono wa kushoto
na viungo vyote hivyo vilitoweka na wahusika wa mauaji hayo” Alisema
Mkumbo.
Alisema
kuwa akiwa amelala nyumbani kwake peke yake mwanamke huyo alivamiwa na
watu wasiojulikana na kuanza kumkatakata mapanga na kuchukua baadhi ya
viungo vyake vya mwili na kutokomea navyo kusiko julikana .
Aliongeza
kuwa katika upelelezi wa awali wa jeshi hilo linawashikiria watu wawili
ambao ni waganga wa kinyeji Gudawa Yalema (52) msukuma na mkulima wa
kijiji hicho.
Alimtaja
mtuhumiwa mwingine kuwa ni Shiwa Masalu (Uselengi) naye mkazi wa kijiji
hicho ambaye alikuwa pamoja na mtuhumiwa wa kwanza wakiwa na vifaa vya
kupigia ramli, huku akieleza chanzo cha tukio hilo ni imani za
kishirikina.
Mkumbo
amewataka wananchi wenye taarifa juu ya wahusika wa tukio hilo kutoa
taarifa hizo kwa jeshi hilo, ikiwa pamoja na kuwataka kutodanganyika
kuwa utajiri unakuja kwa imani za kishirikina, bali unaletwa kwa kufanya
kazi kwa bidii.
Alisema
kuna baadhi ya waganga wanawadanganya wateja wao kuwa viungo vya
mlemavu wa ngozi vinaleta utajiri hali ambayo inawanafanya baadhi ya
watu kuamini na kuendeleza mauaji ya Albino
إرسال تعليق