
Wiki
kadhaa baada ya kumtimua kocha David Moyes klabu ya Manchester united
wanakaribia kumtangaza kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis van Gaal
kuwa meneja mpya wa timu hiyo.Mholanzi huyo tayari ameshakubali
kuchukua madaraka ya ukocha Old Trafford lakini bado ana kazi ya
kuiongoza Uholanzi kwenye michuano ya kombe la dunia na maandalizi ya
kujiandaa na michuano hiyo yamesababisha dili lake na United kuchelewa
kukamilika.Mwanzoni iliripotiwa kwamba angetambulishwa mwishoni mwa wiki
hii lakini badala yake ameendelea kubaki nchini Uholanzi na inaaminika
sasa atatambulishwa wiki ijayo baada ya mchezo wa kirafiki.
Jana Ryan
Giggs ambae ameshika madaraka ya ukocha kwa muda alisafiri mpaka
Uholanzi ambapo alikutana na Van Gaal mjini Noordwijk kwa ajili ya
kuzungumza juu ya Giggs kupewa madaraka ya kocha msaidizi pamoja na
mipango ya usajili msimu ujao.
Post a Comment