Tanzania LEG. Sauti SOL, Radio & Weasel, DJ TIRA ndani ya Billicanas - MTV AFRICA

20140515-123549.jpg

Ikiwa imebaki leo tu kufika ziara ya party ya uhamasishaji wa tuzo za MTV Africa Road to Mama, wasanii kutoka sehemu mbalimbali nje ya Tanzania wanatarajiwa wasili jijini Dar es Salaam siku ya kesho kwa ajili ya maandalizi ya sherehe hiyo itakayo fanyika Club Bilicanas. Wasanii watakao wasili siku ya kesho ni pamoja na ‘Diamond Platnumz Beybe’ aliyepo Uingereza akimalizia Video yake mpya, ‘Professor’ (Afrika Kusini), ‘Sauti Sol’ na ‘Amani’ kutoka Kenya, ‘Radio na Weasel’ wa Uganda ambao wanatarajiwa kupanda jukwaani siku ya Ijumaa ya tarehe 16 Mei ndani ya ukumbi wa club Billicanas.
Mbali na wasanii hao pia ‘DJ Tira’ kutoka Afrika Kusini ambae pia ni DJ wa kituo cha Televisheni cha ‘MTV Base’ nae anatarajiwa kuwasili siku ya kesho kwa ajili ya shughuli hiyo, ataungana na ma DJ wengine wakali kutoka hapa hapa Tanzania ambao watatoa burudani katika sherehe hiyo ya uhamasishaji wa tuzo za MAMA, nao ni pamoja na ‘DJ Zero, DJ Steve B, na DJ Mafuvu’. Sherehe hizo zinalenga kuhamasisha wananchi katika kushiriki kikamilifu katika tuzo hizo na hapa nchini, zitafanyika Club Bilicanas , katika jiji la Dar es Salaam na ticket zitauzwa mlangoni aiku hiyo kwa bei ya shilingi 15,000 kwa mtu moja, mwezi ujao wasanii wataelekea jiji Lagos Nigeria kwa ajili ya uhamasishaji pia.
Vilevile  wasanii  kutoka Afrika Kusini akina ‘Mafikizolo’ na ‘Davido’ wa ‘Nigeria’ wamependekezwa kwenye vipengele vingi Zaidi ya moja, wamependekezwa katika vipengele vinne muhimu, hivyo wameumana katika kuwania tuzo za msani bora wa mwaka pamoja na wimbo bora wa kushirikishwa pia. Pia kutakua na washiriki wawili  ambao ni ‘Radio & Weasel’ kutoka nchini Uganda, na Kenya msanii ‘Amani’ kupitia wimbo wake wa “kiboko changu” alioshirikiana na ‘Radio and Weasel’ nao utashindanishwa.
‘MTV leadership Award’ ni tuzo inayo lenga vijana wa Afrika wanaume na wanawake wenye umri mdogo mpaka miaka 40 ambao wanafanya vizuri kwenye mambo mbalimbali ikiwemo muziki biashara na science. MTV pia inatambua mafanikio ya muziki na wanamuziki ambao wana wakilisha Afrika nchini na inje ya Afrika.
MAMA 2014 itausisha wasanii  wa Afrika na wa Kimataifa pamoja ikiwa pamoja na tuzo ‘sahihi kwa kushirikiana kati ya wasanii wa muziki na tamaduni mbalimbali.
Upigaji kura MTV Africa Awards uko wazi kwenya  www.mtvbase.com kuanzia 16 April 2014 mpaka usiku wa manene  4 Juni 2014.

Post a Comment

Previous Post Next Post