Mohammed Mdose na Said Ally TIMU
za Ligi Kuu Bara zikiwemo Simba na Yanga, huenda zikazuiwa kushiriki
kwenye Ligi Kuu Bara msimu ujao kutokana na kutotekeleza agizo la kuwa
na madaktari wenye vigezo kwenye timu zao.
Agizo hilo lilitolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa nia ya
kuhakikisha kila klabu inakuwa na madaktari waliokidhi vigezo kisha
kuwafanyia vipimo wachezaji wao wote kabla ya kuanza kwa ligi.
Imejulikana kuwa, katika agizo hilo, ni klabu moja pekee kati ya 13 ambayo ndiyo imewasilisha kile ilichoagizwa.
Imejulikana kuwa, katika agizo hilo, ni klabu moja pekee kati ya 13 ambayo ndiyo imewasilisha kile ilichoagizwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tiba ya TFF, Paul Mareale, amesema wamebaini
tatizo hilo baada kupitia wasifu wa kila daktari, hivyo kama
hawatatimiza kigezo hicho hawatairuhusu kushiriki ligi.
“Kumekuwa na madhara makubwa wanayopata wachezaji kutokana na
kutokuwa na wataalam sahihi wa tiba, hatutaki haya yaendelee kujitokeza.
“Msimu huu tupo makini kuhakikisha kila mchezaji hasajiliwi mpaka
afanyiwe vipimo vya afya, tena na daktari mwenye viwango vinavyotakiwa
na TFF, kwa klabu isiyofuata masharti hayo hatutairuhusu kushiriki ligi
kuu.
“Hali hii ya wachezaji kuumia kila siku inatisha, ajabu ni kuwa
hakuna klabu iliyoonyesha kujali zaidi ya Azam. Simba na Yanga
walitakiwa kuwa mifano lakini wao nao hawajaleta chochote, tutawafungia
kwa kuwazuia kushiriki kama wasipotimiza masharti,” alisema.

Post a Comment