MIKAKATI mingi katika kipindi hiki cha usajili mkali na wa umakini zaidi kwa ajili ya msimu ujao inaendele na sasa Simba wamekubaliana kutofanya tena usajili wa gharama wa mamilioni ya shilingi kutokana na sababu mbalimbali.
Mpaka sasa Simba haijafanya usajili wa mchezaji yeyote zaidi ya
kuwatema baadhi ya wachezaji wao huku ikielezwa kuwa, lengo lao ni
kufanya usajili wa siri mno na wa kushtukiza bila ya kuingia kwenye
mvutano na timu yoyote ile.
Imeelezwa kuwa Simba waliweka kikao kwa ajili ya mjadala huo wa
usajili hivi karibuni na wakakubaliana baadhi ya mambo, la kwanza likiwa
ni kutosajili mchezaji yeyote wa Yanga lakini la pili ambalo lilikuwa
bado lipo nyeti ni kutotumia mamilioni kusajili wachezaji kwa kuwa
tathmini inawaonyesha kwamba wachezaji wengi waliowasajili kwa fedha
nyingi hawana msaada na timu hiyo.
Chanzo cha makini kutoka ndani ya Simba kimesema
kuwa, bado viongozi wa timu hiyo ambao wana uhakika wa kubaki
madarakani mara baada ya uchaguzi, wanaendelea kuangalia ni vijana gani
watakaowafaa zaidi klabuni hapo bila ya kutumia pesa nyingi.
إرسال تعليق