Dar es Salaam. Taasisi ya Afya ya Ifakara kwa
kushirikiana na ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa, wameamua kuanza kuchukua
sampuli za damu za wagonjwa wanaohisiwa kuwa na maambukizi ya homa ya
dengue na kwenda kuzifanyia vipimo katika ofisi ya Mkemia Mkuu.
Uamuzi huo umekuja kutokana na kuadimika kwa
vipimo vya ugonjwa huo, sambamba na taasisi hiyo kumaliza muda wake wa
kufanya utafiti kuhusu sababu za homa kwa mtu asiye na ugonjwa wa
malaria.
Akizungumza jana, Mganga Mkuu wa Hospitali ya
Rufaa ya Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani alisema katika kikao
kilichofanyika jana na Mganga Mkuu wa Mkoa, ambacho walifikia maazimio
kwamba sampuli za wagonjwa wenye viashiria vya dengue zichukuliwe kwa
ajili ya vipimo katika maabara kuu ya taifa.
“Tumekaa kikao leo (jana) na Mganga Mkuu wa Mkoa,
tumeazimia kwamba vipimo vitaendelea lakini kwa sasa tutachukua damu za
wagonjwa na kupeleka maabara ya taifa, ambako zitapimwa na majibu
yatarudi baada ya siku mbili. Hii inatokana na kumalizika kwa vipimo
kutoka taasisi ya Ifakara Health Institute,” alisema Dk. Ngonyani.
Alisema umewekwa utaratibu maalumu jinsi ya
kusafirisha sampuli hizo za damu kwa ajili ya kwenda kufanyiwa vipimo na
kurudisha majibu yake baada ya kukamilika.
Ngonyani alisema kumalizika kwa utafiti huo,
hakutaizuia taasisi hiyo kuendelea kutoa huduma kwani wamekwishaagiza
vipimo vingine ambavyo vinatoka nje vinavyotarajiwa kuwasili keshokutwa.
Daktari Kiongozi na Mtaalamu wa homa ya dengue Dk.
Mrisho Lupinda alisema utafiti wao ulikamilika Jumatano, lakini
kutokana na ukubwa wa tatizo wataendelea na zoezi hilo.
“Kulingana na utafiti wetu, tulikuwa na namba
kamili ya watu ambao tulihitaji kuwafanyia utafiti huu na namba hiyo
ilishakamilika hapo ndipo tukamaliza zoezi letu, lakini tunaendelea na
zoezi hili na Jumatatu. Vipimo vingine vitawasili ambavyo vimeagizwa nje
ya nchi na tunaamini kwamba vitaendelea kusaidia wagonjwa mbalimbali wa
homa hii,” alisema Lupinda.
Hata hivyo Lupinda alitoa wito kwa wagonjwa
mbalimbali kukubali kupima vipimo vyote kwanza, kabla ya kukimbilia
kipimo hicho kwani kina gharama kubwa.
“Kuanzia sasa mgonjwa yeyote atakayefika hospitali
atalazimika kupima vipimo vyote ili tubaini iwapo ana malaria au homa
ya aina nyingine, kabla ya kukimbilia kupima dengue. Hii itasaidia kuwa
makini na kupunguza gharama ambayo ingeweza kupotea na gharama hiyo
imfae mtu mwingine,” alisema Lupinda.
Gharama ya vipimo
إرسال تعليق