Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dar es Salaam Hassan Kaumo akiongea na wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ni Fanuel Mbonde. (Picha na Martha Komba - Wizara ya Katiba na Sheria).
Na Martha Komba, Dar es Salaam
Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde amesema hayo
katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika jana
jijini Dar es Salaam.
“Uwajibikaji
ni suala muhimu sana katika utumishi wa umma,” alisema katika mkutano
huo wa siku moja uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es
Salaam.
Aidha,
Katibu Mkuu huyo aliwasihi watumishi wote wa Wizara yake kuungana na
wafanyakazi wote nchini na duniani kushiriki katika sherehe za Siku ya
Wafanyakazi zinazofanyika Mei 1, 2014.
Awali akiongea katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dar es Salaam Hassan Kaumo aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kutimiza wajibu wao katika sehemu zao za kazi.
“Tunapodai
maslahi ni lazima pia tusisitize kutimiza wajibu. Wafikishieni salamu
hizi wafanyakazi wote, wachape kazi ili watupe viongozi nguvu ya kudai
maslahi bora,” alisema Kaumo katika mkutano huo uliohudhuriwa na
viongozi na wawakilishi wa wafanyakazi kutoka Idara na Vitengo vyote vya
Wizara hiyo.
Mkutano
huo, pamoja na mambo mengine, ulijadili maslahi ya watumishi na kupitia
na kuridhia Taarifa ya Mpango wa Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka ujao
wa fedha 2014/2015.
إرسال تعليق