
Asilimia
36 ya watu wanaotumia dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga sindano nchini,
wana maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Takwimu
hizo huenda zikaongezeka, ikiwa jamii haitaelimishwa jinsi ya kupunguza
madhara dhidi ya dawa hizo.
Hayo
yalisemwa jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Mtandao wa Watu wanaotumia
Dawa za kulevya (TanNPUD), Happy Assen kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa
ya Kupunguza Madhara kwa watumia dawa za kulevya.
Alisema
ingawa matumizi ya dawa za kulevya ni makubwa nchini, bado jamii haiko karibu
na watu wanaotumia dawa hizo, na badala wametengwa kama wahalifu, na kusahau
kwamba nao pia ni sehemu ya jamii na wanapaswa kusaidiwa.
“Wanajamii
wana mtazamo hasi kuhusu upunguzaji madhara kwa watumia dawa za kulevya, wengi
wanadhani upunguzaji madhara unachangia ongezeko la matumizi ya dawa hizo
kwenye soko, jambo ambalo sio sahihi,” alisema Assen.
Alisema
takwimu za afya na matumizi ya dawa za kulevya nchini, zinaonesha asilimia 36
ya watumia dawa za kulevya nchini kwa njia ya kujidunga sindano, wamepata
maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Alisema
hiyo inatokana na watumia dawa hizo, kuchangia bomba moja la sindano watu wengi
wakati wa kujidunga dawa za kulevya aina ya heroine, kwa sababu hawana uwezo wa
kumudu gharama za kununua kila mmoja bomba lake.
Takwimu
za hivi karibuni nchini za matumizi ya dawa za kulevya, zinaonesha kwamba
watu wanaotumia dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga sindano ni 25,000, na
kati ya hao 18,000 wapo Dar es Salaam.
Alisema,
TaNPUD kwa kushirikiana na wataalamu wa masuala ya Video na Afya ya
Maendeleo(VAMA), wameandaa onesho litakalofanyika jijini Dar es
Salaam kwa lengo la kuwaelimisha wananchi kuhusu upunguzaji madhara kwa
watumia dawa za kulevya, ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
إرسال تعليق