MUNGU mkubwa! Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila
‘Ray C’, amesimulia jinsi alivyochungulia kifo baada ya kutikiswa na
ugonjwa hatari na tishio ulioibuka hivi karibuni wa Homa ya Dengue.

Akifunguka mbele ya gazeti hili juzi baada ya kuruhusiwa kutoka
hospitalini Mwananyamala, Dar alikokuwa amelazwa, Ray C au Kiuno Bila
Mfupa alisema kwamba kwenye maisha yake hajawahi kushikwa na ugonjwa
wenye mateso makali, tena ya muda mfupi kama ilivyokuwa juzikati
alipopata ugonjwa huo.
Alisema kwamba dakika chache tu baada ya kuamka kitandani alikuwa
akijisikia kichwa kikiuma kama kinataka kuchomoka ambapo bila kuremba
aliwasha gari lake na kukimbilia Hospitali ya Mwananyamala.
Staa huyo wa Ngoma ya Na Wewe Milele alisema alipofika kwa kudra za muumba alilazwa tayari kwa kutundikwa dripu.

“Madaktari wengine wakatishika zaidi maana walisema kama ukimeza vidonge vya ‘Diclopa’ unaweza kupoteza maisha mara moja.
“Katika magonjwa ya ajabu na yanayostahili kutafutiwa kinga mara moja
basi huu ni ugonjwa wa kwanza ambao serikali inatakiwa iwe macho sana
maana haufai hata kidogo.
“Tena unatisha sana na wasipoangalia utapoteza maisha ya Watanzania kibao kama hawatautafutia kinga au kuwapa Watanzania elimu ya kutosha.
“Tena unatisha sana na wasipoangalia utapoteza maisha ya Watanzania kibao kama hawatautafutia kinga au kuwapa Watanzania elimu ya kutosha.
“Mateso niliyoyapata kwa siku mbili nilizolazwa Mwananyamala ni elimu
tosha kabisa na kwamba ningekuwa na uwezo wa kuzunguka au kupata nafasi
ya kuongea na wakuu wa nchi basi mara moja ningewaomba wafanye jitihada
za haraka kuhakikisha wanapata chanjo kwa ajili ya kuudhibiti mfumko wa
gonjwa hilo.
“Dengue unaambukizwa na mbu tena wa mchana na dawa yake ni panadol tu!” alimalizia Ray C.
إرسال تعليق