Hivi Ndivyo Wasanii walivyompongeza Diamond kwa nomination ya BET Awards .


Baada ya Diamond Platnumz kuwa msanii wa kwanza wa Tanzania kuwahi kutajwa kuwania tuzo za BET, wasanii mbalimbali nchini wamempongeza huku Ben Pol akisema amewatiwa watu imani juu ya muziki wa Tanzania.
benpol(2)
Akizungumza na Bongo5 leo,Ben Pol amesema huu ni wakati wa Watanzania kujivunia nafasi hiyo ambayo itaitangaza Tanzania na muziki wake katika ramani ya kimataifa. “Unajua umefika muda wa kukubali juhudi za mtu mwingine. Kwenye kitu kama hiki ambacho amefanya mshkaji (Diamond) ninaweza kusema ametutengenezea imani,yaani kuaminika, kwasababu nafikiri ndio msanii wa kwanza wa Tanzania kupata Nomination za BET Awards. Kwahiyo hiki ni kitu kikubwa sana sana, na tunatakiwa kuwa proud kama Tanzania wanakusupport,” amesema.
Wasanii na mastaa wengine wamempongeza staa huyo kupitia mitandao ya kijamii.
AY
Congraaaaaats @diamondplatnumz kwa kuchaguliwa kwenye BET Awards 2014…Tanzania Stand Up!!!!Tutavote mpaka mzigo uje home #BONGOFLAVA

Professor Jay
Congratulations mwanangu @diamondplatnumz … Tunapambana mpaka kieleweke. . BET STYLE BEIBEE!! Bongo TZ Stand up!!!

Ommy Dimpoz
This Happening now after BET AWARDS NOMINATION shiiiiiityyy Africa Stand up!!! Proudly Tanzania thank u my nigga @diamondplatnumz kwa kutuweka kwenye Ramani

Post a Comment

Previous Post Next Post