Mholanzi, Hans van Der Pluijm.
KAMATI ya usajili ya Yanga kwa sasa imesimama kutafuta wala kufanya usajili wa wachezaji wa kigeni kutokana na kuamua kufuata maagizo ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van Der Pluijm.
Hatua ya kusimama kufanya usajili huo, inakuja baada ya viongozi wa
Yanga kutii na kuheshimu kauli iliyotolewa na Pluijm kuwa atawaletea
kifaa kitakachokuwa msaada, hivyo maamuzi yote juu ya usajili wa
mchezaji wa nje yanasubiri jina litakalotumwa na kocha huyo.
Tayari Mholanzi huyo yupo Ghana kwa ajili ya zoezi hilo na akishamaliza shughuli hiyo, anatarajia kujiunga na Al Shoala mara moja kwa ajili ya kuanza kazi.
Tayari Mholanzi huyo yupo Ghana kwa ajili ya zoezi hilo na akishamaliza shughuli hiyo, anatarajia kujiunga na Al Shoala mara moja kwa ajili ya kuanza kazi.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, amesema kwamba kwa sasa Yanga
imetulia kuhusu usajili wa nje na sababu kubwa ni kutimiza ahadi hiyo
kwani wanasubiri tamko la kocha huyo wa zamani wa Berekum Chelsea ya
Ghana.
Hata hivyo, Njovu alifafanua kwamba si lazima kocha huyo atafute
mchezaji kutoka kwenye Ligi Kuu ya Ghana au awe raia wa Ghana, isipokuwa
amekwenda huko kwa kuwa kuna ‘connection’ nyingi.
“Wakati anaondoka kwa ajili ya kwenda kufanya shughuli hiyo, alituambia kwamba ameshakisoma kikosi vizuri ndani ya miezi sita, kwa hiyo anajua amlete mchezaji wa aina gani ili kikosi kiwe bora zaidi msimu ujao, ndiyo maana tunamsubiri yeye kuhusu usajili wa nje.

“Lakini hata kama yupo Ghana haimaanishi kwamba ni lazima ataleta
mchezaji wa Ghana, anaweza kusajili wengine ila anaamini akiwa hapo
anaweza kuwapata na wengine wa nchi nyingine kutokana na uzoefu wake,”
alisema Njovu na kuongeza:
“Unajua mchezaji wa nje anayetakiwa hapa ni mmoja tu kwa ajili ya
kukamilisha hesabu za wachezaji watano, tayari tunaye Haruna Niyonzima,
Mbuyu (Twite), Okwi (Emmanuel) na Kiiza (Hamis), kwa hiyo anasubiriwa
huyo tu, tufunge masuala ya usajili wa huko nje.”
Imeelezwa kuwa, Pluijm anaweza kumpotezea kiungo wa Ghana, Joseph Zuttah, aliyekuwa na malengo naye ya kumleta Jangwani tangu awali, baada ya kupewa taarifa kwamba kwa sasa ni mtovu wa nidhamu.
Imeelezwa kuwa, Pluijm anaweza kumpotezea kiungo wa Ghana, Joseph Zuttah, aliyekuwa na malengo naye ya kumleta Jangwani tangu awali, baada ya kupewa taarifa kwamba kwa sasa ni mtovu wa nidhamu.
إرسال تعليق