‘Die hard fans’ wanaweza kufanya lolote kuhakikisha wanampa
ushindi msanii wao katika shindano lolote linalohiotaji ushiriki wao
hasa wa kupiga kura au maoni, kama kinachofanywa hivi sasa na mashabiki
wa Diamond Platnumz katika tuzo za BET.

BET wanaendelea kuweka majina ya nominees katika page zao za
mitandao ya kijamii ili kuwapa mashabiki nafasi ya kuwaongezea
ushawishi wa kupewa ushindi wasanii wao. Kama ilivyokuwa jana picha ya
Diamond imeendelea kupata likes na comments nyingi katika Facebook ya
BET, mpaka sasa ina likes 2649 na comments 5471 huku Davido akiwa na
likes 1465 na comments 619 tu.
Upande wa Instagram ya BET Awards picha ya Diamond iliyowekwa jana usiku na maelezo haya:
‘Dbl tap this pic if you want #DiamondPlatnumz to win #BestInternationalAct: Africa @ the #BETAwards this yr’,
Hadi sasa ina likes 3275 na comments 4354 huku picha ya Davido katika akaunti hiyo ya IG ya BET iliyowekwa siku mbili zilizopita ina likes 518 na comments241 tu.
Hadi sasa ina likes 3275 na comments 4354 huku picha ya Davido katika akaunti hiyo ya IG ya BET iliyowekwa siku mbili zilizopita ina likes 518 na comments241 tu.

Cha kushangaza mashabiki wa Diamond wameamua kutoka nje ya kile
kinachotarajiwa baada ya kuamua ku-comment jina la Diamond katika picha
hiyo ya Davido.
Post a Comment